Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Samwel Msanjila (wapili kushoto) akielezwa jambo na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Chuma wa Kumaraswamy uliopo Vijaynagar katika Jimbo la Karnataka, India, Bwana Sunil Kumar alipotembelea Mgodi huo tarehe 11 Juni, 2019 wakati wa ziara ya Mafunzo nchini India. Mgodi huo wa Chuma unamilikiwa na Shirika la Taifa la Madini nchini India (NMDC).
Katika ziara hiyo, Prof. Msanjila aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Kanali Sylivester D. Ghuliku, Kamishna Msaidizi wa Madini, Dr. Godfrey Nyamrunda na Mkurugenzi wa Leseni za Madini katika Tume ya Madini, Eng. Yahya Samamba.