Tarehe 24 Septemba, 2019 Ubalozi wa Tanzania, New Delhi uliendesha Kikao cha Kwanza cha Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika [SADC] chini ya Uenyekiti wa Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka H. Luvanda.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Luvanda aliwakaribisha rasmi Mabalozi wenzake na Maafisa walioambatana nao katika jengo linalomilikiwa na Serikali ya Tanzania Jijini New Delhi [Tanzania House].

Jumla ya Mabalozi 8 walishiriki kikao hicho ambapo 6 walikosekana kwa udhuru mbalimbali. Kubwa lililojitokeza lilikuwa ni kujadili namna ya utekelezaji wa Maazimio na maelekezo yaliyotokana na Mkutano wa 39 wa kilele wa Viongozi Wakuu wa Serikali na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam, Tanzania tarehe 17-18 Agosti, 2019 chini ya Uenyekiti wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mkutano huo uliazimia kuanza utekelezaji huo mara moja.

  • Mhe. Balozi Luvanda akimkaribisha Balozi wa Msumbiji nchini India, Mhe. E. A. Ferreira Ubalozini, New DelhiMhe. Balozi Luvanda akimkaribisha Balozi wa Msumbiji nchini India, Mhe. E. A. Ferreira Ubalozini, New Delhi
  • Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Zambia nchini India, Mhe. Judith K. Kapijimpanga ambaye kabla ya kuiwakilisha Zambia nchini India, alihudumu katika nafasi hiyo nchini Tanzania.
  • Mhe. Balozi Luvanda akikabidhiwa Makabrasha ya Mwenyekiti wa Kundi la Mabalozi wa nchi za SADC aliyemaliza muda wake, Balozi wa Namibia nchini India, Mhe. Gabriel P. Sinimbo.
  • Kikao kikiendeleaKikao kikiendelea
  • Maafisa Ubalazo wa Tanzania, New Delhi Dkt. Kheri Goloka [kushoto] na Bi. Natihaika Msuya [katikati] wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa kundi la Mabalozi wa chi za SADC nchini India aliyemaliza muda wake, Balozi wa Namibia nchini India, Mhe. Gabriel P. Sinimbo
  • Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamojana na Mabalozi pamoja na Maafisa Ubalozi wa chi za SADC nchini India wakati wa Kikao cha Mabalozi wa Nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika [SADC] kilichofanyika tarehe 24 Septemba, 2019 katika jengo la Ubalozi, Jijini New Delhi