Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini wa India, Bibi Rasika Chaube akisisitiza jambo alipokuwa kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon S. Msanjila, New Delhi tarehe 13 Juni 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon S. Msanjila akimpatia zawadi ya kitabu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini wa India, Bibi Rasika Chaube kinachoonesha maeneo mbalimbali yenye madini nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon S. Msanjila wa (pili kulia) akiwa na ujumbe wake aliongozana nao katika ziara ya mafunzo nchini India. Kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Madini, Dkt. Godfrey Nyamrunda, anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO), Kanali Sylivester D. Ghuliku na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Leseni za Madini katika Tume ya Madini, Eng. Yahya Samamba.
Prof. Msanjila (katikati) na ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo. Kutoka kulia ni Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini India, Dkt. Kheri Goloka, Mkurugenzi wa Leseni za Madini katika Tume ya Madini, Eng. Yahya Samamba anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Kanali Sylivester D. Ghuliku na wa mwisho kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Dkt. Godfrey Nyamrunda
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Samwel Msanjila (wapili kushoto) akielezwa jambo na Meneja Mkuu wa Kituo Cha Utafiti wa Madini kinachomilikiwa na Shirika la Taifa la Madini nchini India (NMDC) kilichopo Hyderabad katika Jimbo la Telangana, India, alipotembelea Kituoni hapo tarehe 14 Juni, 2019 wakati wa ziara ya Mafunzo nchini India. Katika ziara hiyo, Prof. Msanjila aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Kanali Sylivester D. Ghuliku, Kamishna Msaidizi wa Madini, Dr. Godfrey Nyamrunda na Mkurugenzi wa Leseni za Madini katika Tume ya Madini, Eng. Yahya Samamba.
Prof. Msanjila na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.
Prof. Msanjila na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Samwel Msanjila (wapili kushoto) akielezwa jambo na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Chuma wa Kumaraswamy uliopo Vijaynagar katika Jimbo la Karnataka, India, Bwana Sunil Kumar alipotembelea Mgodi huo tarehe 11 Juni, 2019 wakati wa ziara ya Mafunzo nchini India. Mgodi huo wa Chuma unamilikiwa na Shirika la Taifa la Madini nchini India (NMDC). Katika ziara hiyo, Prof. Msanjila aliambatana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Kanali Sylivester D. Ghuliku, Kamishna Msaidizi wa Madini, Dr. Godfrey Nyamrunda na Mkurugenzi wa Leseni za Madini katika Tume ya Madini, Eng. Yahya Samamba.
Matukio ya Ziara ya Wataalam wa Wizara ya Madini nchini India
