Balozi Baraka H. Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ujumbe wa washiriki wa mafunzo kutoka Chaneli ya Utalii Tanzania ambao wapo nchini India kwa ziara ya mafunzo. Ujumbe huo unaongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania [TBC], Dkt. Ayub Rioba Chacha na Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas.