Ili kuweza kufanya maombi ya Hati ya Dharura, ,
Mwombaji anatakiwa kuwa na vielelezo vifuatavyo:-

• Cheti Chake cha Kuzaliwa;

• Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa mmoja wa wazazi wake;

• Picha ya (Passport Size) yenye rangi ya bluu bahari nyuma;

• Vielelezo vya Ushahidi wa Safari;

Barua ya maombi ya Hati ya Dharura (ielekezwe kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, S.L.P 512, Dar Es Salaam);

NB:

* Viambato vyote ni lazima viwe kwenye mfumo wa PDF na kila Kiambato kisizidi ukubwa wa Kb 1032*

* Picha (Passport size) ya Muombaji yenye rangi bluu bahari nyuma, iwe kwenye mfumo wa JPG ,PNG au JPEG

*Unasisitizwa Kunakiri Namba yako ya ombi pindi atumapo ombi kwa ajili ya kumbukumbu*
*Fomu ichapwe katika fomati ya A4*