HATUA ZA UOMBAJI E-PASSPORT

Kabla ya kujaza Fomu Mwombaji ahakikishe anaskani picha yake (passport size) na viambatanisho vyote (Cheti cha kuzaliwa, nakala ya pasipoti, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo (affidavit] ya Baba au Mama mzazi wa mwombaji mwenye uraia wa Tanzania na kitambulisho cha uraia kama anacho). Viambatanisho hivyo viwe kwenye mfumo wa picha (image. jpeg, jing) na kila kiambatishi kisizidi ukubwa wa 1 MB. Viambatanisho hivyo atatakiwa kuvipakia (upload) wakati anajaza fomu.

Awe na kadi yake ya benki ambayo atatumia kufanya malipo wakati wa kujaza fomu hiyo.

Kwa waombaji walio miji ya mbali watatakiwa kutuma Ubalozini gharama za kutuniwa pasipoti zao zikifika Ubalozini. Gharama hizo zitumwe kwa njia ya “Demand Draft”.

 

Mwombaji ajaze fomu katika mtandao (online) kupitia kwenye tovuti ya Idara ya Uhamiaji https://www.immigration.go.tz  ataona sehemu ya kupata fomu ya maombi ya pasipoti (passport application form)

Atatoa nakala ya fomu ya maombi pamoja na viambatisho vyake na kuituma kwa parua pepe ifuatayo: epassport@tanzrepdelhi.com

Ikishapokelewa na kuthibitishwa na Ubalozi muombaji atatumiwa Ankara (bill) ya malipo katika anuani ya barua pepe aliyojaza kwenye fomu ya maombi ya pasipoti

Ankara hiyo ya malipo itamwonyesha “link” ya kufanya malipo kwa njia ya mtandao  https://epay.gepg.go.tz

Kwenye “link” hiyo ataweka namba ya udhibiti (control number) na kiasi cha malipo kama Ankara (bill) inavyoonesha

Akikamilisha malipo atume risiti yake Ubalozini ili malipo yahakikiwe na kupangiwa miadi ya kuja Ubalozi kwa ajili ya kupiga picha pamoja na kuchukuliwa alama za vidole

Wakati anakuja Ubalozini ahakikishe anakuja na nakala halisi za viambatisho vyake pamoja na fomu ya maombi ya rangi (coloured printed application form) na atapatiwa risiti yake ya malipo

Pasipoti ikipokelewa kutoka Uhamiaji, Dar es Salaam, mhusika atatumiwa kwa njia ya posta (courier) au kuchukua mwenyewe Ubalozini.

 

 

 

UBALOZI WA TANZANIA, NEW DELHI, INDIA

MEI 2019