tanzania high commission - new delhi

UTANGULIZI;
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, akiuongoza Ujumbe wa watu watano, aliwasili India, tarehe 2 Oktoba, 2012 kwa lengo kuhudhuria Mkutano wa “Inter-Parliamentary Union Women Speakers Conference” uliofanyika New Delhi kuanzia tarehe 3 na 4 Oktoba, 2012 .

Pamoja na shughuli hiyo, Mhe. Spika alipata fursa ya kuutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India na kusalimiana na Balozi pamoja na Maafisa wengine wa Ubalozi.

Ziara ya Mhe. Spika na Ujumbe wake katika Ubalozi, ilianza kwa kutembelea Ofisi na kupata maelezo ya maeneo mbali mbali ya Jengo la Ubalozi kabla ya kutia saini kitabu cha wageni na baadae kuwa na mazungumzo/mkutano na Maafisa wa Ubalozi wazalendo.

tanzania high commission - new delhi

MAZUNGUMZO:
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini India, Mhe. Eng. John W. H. Kijazi,
kabla ya kueleza kwa muhtsari taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi katika  utekeleza Sera ya Taifa ya Diplomasia ya uchumi pamoja na kuendeleza mbele uhusiano na ushirikiano mwema baina ya Tanzania na India, alichukua fursa kwa niaba ya Maafisa wengine wa Ubalozi kumpongeza kwa dhati Mhe. Spika kwa kuteuliwa kwake kushika wadhifa huo.

Alisema Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania New Delhi wanaungana na Watanzania wengine pamoja na wapenda amani wote duniani kumpongeza Mhe. Anne Makinda ambaye amekuwa ni mwanamke wa kwanza katika historia ya Tanzania kushika wadhifa huo adhimu.

tanzania high commission - new delhi

Mhe. Balozi aliendelea kusema kwamba uteuzi wa Mhe. Makinda, ambaye alishawahi kuwa Naibu Spika haukuwa wa kubahatisha, bali unatokana na juhudi katika kazi, utendaji mzuri pamoja na ushirikiano wake wa karibu na Wabunge wenzake ndio uliolipelekea Bunge kuona umuhimu mkubwa wa kumpa Mhe. wadhifa huo likiwa na yakini kwamba anaweza kuutekeleza kwa ufanisi mkubwa.

Alisema katika kipindi kifupi tangu kushika wadhifa huo, Mhe. Spika ameweza kuliongoza na kulielekeza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa makini na kutekeleza kwa dhati jukumu lake muhimu la kushauri na kusimamia utendaji wa Serikali na kwamba mfano hai wa mabadiliko hayo yenye bashira njema kwa maendeleo ya Bunge na taifa kwa jumla ni yaliyojiri wakati wa kikao cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

tanzania high commission - new delhi

TAARIFA YA UBALOZI
Mhe. Balozi Kijazi alieleza kwa muhtasari maendeleo yaliyopatikana katika uhusiano mwema uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 baina ya Tanzania na India katika Nyanja zotezikiwemo siasa, uchumi, utamaduni, teknolojia na jamii.

tanzania high commission - new delhi

Aidha alimuelezea Mhe. Spika na ujumbe wake juu ya utekelezaji wa majukumu na juhudi mbali mbali za Ubalozi katika kuiwezesha Tanzania kunufaika kupitia Diplomasia ya Uchumi katika eneo hili, kuimarisha ushirikiano katika sekta za ulinzi na afya pamoja na changamoto mbali mbali zinazoukabili Ubalozi katika kuyatekeleza hayo ikiwemo changamoto sugu ya ufinyu wa bajeti.

tanzania high commission - new delhi

TAARIFA YA MHE. SPIKA:
Mhe. Spika wa Bunge la Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, alianza kwa kutoa shukrani zake kwa Mhe. Balozi na Maafisa wake kwa mapokezi mazuri, ukarimu pamoja na kuwaandalia taarifa hii ambayo imewapa mwanga kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo katika eneo hili pamoja na maendeleo makubwa yaliyopatikana ndani ya ushirikiano wa India na Tanzania. Aidha, Mhe. Spika alimpongeza sana Mhe. Balozi na Maafisa wake kwa kuwa wastahamilivu na kujizatiti kutekeleza majukumu ya Ubalozi licha ya changamoto mbali mbali zinazowakabili.

tanzania high commission - new delhi

Akizungumzia, changamoto zinazoukabili Ubalozi wa Tanzania nchini India ambazo ni sawa na Balozi zote za Tanzania nchi za nje, Mhe. Spika, alisema kwamba Bunge limegundua kwamba Sera ya Diplomasia ya Uchumi ambayo ni msingi mkubwa maendeleo ya uchumi wa Taifa letu haitekelezeki kwa sababu haikupewa umuhimu inayostahili na kwa mantiki hiyo Bunge la Jamhuri yam Tanzania limo katika mchakato [studies] wa kutafuta mbinu za kuzifanya Balozi
zetu kuwezeshwa kutekeleza kikamilifu Sera ya Diplomasia ya Uchumi katika maeneo yao.

Alisema mojawapo wa juhudi za Bunge katika kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala hilo, ni ile ziara ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea baadhi ya Balozi kukusanya taarifa za kuzifanyia kazi. Mhe.Spika aliendelea kusema kwamba Bunge limeunda Kamati ndogo ndogo zinazoendelea kufanya utafiti [study] kuhusu makusanyo ya Serikali [revenue] na na Sekta ya afya na kwamba zinatarajiwa kutoa taarifa na mapendekezo yake baada ya miezi sita.

tanzania high commission - new delhi

Vile vile Mhe. Spika alizungumzia juu ya hatua za Bunge katika kuboresha sheria inayosimamia haki za Wabunge na maadili [ethics] ya Bunge. Alisema japokuwa Sheria ipo na kwamba Bunge lina utaratibu wa kutoa semina [induction] kwa Wabunge wapya, lakini bado ipo haja ya sheria hiyo kuangaliwa upya ili iendane na wakati uliopo na vile vile iweze kuthibiti vyema maadili ya Bunge.

Wakichangia taarifa hiyo ya Mhe. Spika, Mhe. Balozi pamoja na Maafisa wa Ubalozi, wameshauri kwamba Serikali iangalie upya sheria na taratibu zinazomruhusu Mtanzania kugombea Ubunge, ili iweze kusimamia upatikanaji wa Wabunge madhubuti ambao watakuwa na moyo wa kujituma, kuthamini cheo na dhamana wanazopewa na wananchi kwa kuyawakilisha vyema majimbo yao, badala ya kuchukulia Ubunge kama ajira au njia mbadala  a kujipatia mali kwa haraka.