Tarehe 09 Disemba 2021 Ubalozi wa Tanzania, New Delhi ulisherehekea kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania katika Hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Taj Mahal, jijini New Delhi.

Mabalozi wa nchi mbalimbali, viongozi wa taasisi za umma na watu binafsi, wafanyabiashara, diaspora wa Tanzania, India pamoja na wanafunzi waliudhuria. Maadhimisho hayo yalipambwa na shughuli mbalimbali, zikiwemo; maonyesho ya bidhaa na vivutio vya utalii vya Tanzania, ngoma za asili, uzunduzi wa Jarida mahsusi lililoandaliwa na Ubalozi kuhusu miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania (Tanzania At 60)  likiwa limesheheni taarifa zinazohusu fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na kutangaza vivutio vya utilii.