Tanzania imeshiriki kwa mafanikio katika maonesho makubwa kabisa ya utalii barani Asia yanayojulikana kama OTM. Maonesho hayo yamefanyika Mumbai, India tarehe 30 Januari hadi 1 Februari 2025. Ubalozi wa Tanzania, kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na kampuni ya utalii ya SWAHILI Safaris kwa Pamoja wamewezesha ushiriki wa wadau 19 kutoka sekta binafsi na taasisi za umma.
 
Wadau wafuatao walishiriki maonesho hayo:
1.   Tanzania Tourist Board (TTB) @TTBTanzania 
2.   Swahili Safaris
3.   Tanzania Investment Centre (TIC) 
4.   Mauly Tours
5.   Tanzania Forest Services Agency (TFSA)
6.   Safari Gateway
7.    Dolphin – Tours & Safari Ltd
8.   ODA Tours Safari
9.   Zanzibar Commission for Tourism (ZCT)
10. ZAFS Tours
11.  Inquisitive Africa – Safari & Adventure
12.  Tanzania National Parks (TANAPA)
13.  Ngorongoro Conservation Area Authority 
14.  Bluebay Beach Resort & Spa
15.  SIMBA Portfolio
16.  BABII Tours & Safaris Ltd
17.  The Safari Artist
18.  SVAI Luxe Escapes
19.  ASANJA