Ubalozi umepokea taarifa toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhusu utaratibu ambao Diaspora wanaweza kutumia kufanya usajili wa vitambulisho vya Taifa.

Mamlaka imemteua Bi. Lilian Kowelo, kuwa Afisa Usajili atakae shughulikia masuala ya diaspora ndani ya mamlaka ya NIDA. Dawati hili litatoa huduma kwa haraka kwa diaspora katika jengo la ofisi za Posta Mpya (One Stop Center), Dar es-Salaam.

Kwa maelezo zaidi wasiliana moja kwa moja na Bi. Lilian Kowelo kupitia namba ya simu: +255 712557706 au kwa barua pepe: lilian.kowelo@nida.go.tz

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya  NIDA