Uhakiki wa taarifa za Watanzania waliokwama India

1. Dhumuni  la fomu hii ni kuhakiki taarifa za raia wa Tanzania waliokwama nchini India.

2. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakamisha mchakato wa kutuma tena ndege Maalum kuja kuwachukua raia wa Tanzania waliokwama nchini India ambao walishindwa kusafiri na ndege maalum zilizotumwa nchini India kutokana na sababu mbali mbali. Ubalozi unaomba mchangamkie fursa hii adhimu maana hakutakuwa na ndege nyingine maalum itakayotumwa tena India kwa shughuli hii.

3.Taarifa kuhusu gharama za tiketi, namna ya kulipia tiketi hizo, namba ya akaunti ya benki ya kufanya malipo ya tiketi zitawekwa kwenye tovuti ya Ubalozi.

4. Fomu hii inatakiwa kujazwa na kila mtu anayekusidia kusafiri kurudi Tanzania kwa kutumia ndege hiyo maalum. Aidha, kama hupo na familia, utalazimika kujaza fomu tofauti kwa kila mwanafamilia.

5. Mara tu, ujazapo fomu hii na kuiwasilisha [submit], itapokelewa na Ubalozi, hivyo hauna haja ya kuituma tena kwa njia ya barua pepe au njia nyingine yeyote.

6. Ubalozi utawasiliana nawe moja kwa moja endapo kutakuwa na sababu ya kufanya hivyo.

7. Pakua fomu    hapa