• Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Singapore Mhe.Teo Sieng Seng mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changi Nchini Singapore. Makamu wa Rais yupo Nchini Singapore kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Majadiliano ya Kiuchumi (Bloomberg New Economy Forum 2021 ). Novemba 15,2021.