India ni nchi ya pili duniani [baada ya Jamhuri ya Watu wa China] ambayo uchumi wake unakua kwa kasi sana. Uchumi wa nchi hii ulirekodiwa kukua kwa wastani wa asilimia 8.9  katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2010/11  na kasi hiyo ambayo inachangiwa na ustawi wa sekta za kilimo, viwanda na huduma iliongezeka hadi kufikia silimia 9 katika robo ya tatu na nne ya mwaka huo.

Licha ya ukuaji huo India bado ina mahitaji mengi na inaendelea kuagiza malighafi, utaalamu na bidhaa kutoka nchi mbali mbali duniani. Miongoni mwa mahitaji hayo ni bidhaa za mitaji, mafuta [fuel], mafuta ya kupikia, mbolea, nafaka [hasa jamii ya kunde na maharage - Pulses], madini ya chuma na madini ya aina nyingine, mashine za viwandani, vifaa vya kitaalamu, vifaa vya usafirishaji, kemikali,vito vya thamani nk. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/12, India ilitumia jumla ya Dola Milioni 3,5371 kwa uagiziaji [import].

Mauzo ya Tanzania kwa India- Tanzania inauizia India mazao ya kilimo kama korosho, pamba, kahawa, chai, viungo, ngozi za wanyama nk: bidhaa za misitu zikiwemo mbao na bidhaa za madini na vito vya thamani zikiwemo dhahabu, almasi nk.

Mauzo ya India kwa Tanzania - India inauizia Tanzania bidhaa  mbali mbali zikiwemo mashine, bidhaa za nguo, zana za kilimo, zana za usafirishaji, madawa, vifaa vya ujenzi, nafaka, bidhaa za matumizi, mitaji nk.

Tanzania ina nafasi kubwa ya kutumia mwanya huo ili kuongeza mauzo yake nchini India hasa mazao ya kilimo. India ni mlimaji na mtumiaji mkubwa wa nafaka aina ya pulses [mbaazi, kunde choroko nk.] ambazo zinapatikana kwa wingi Tanzania. mwaka 2011 iliagiza Tani 350,000 za pulses kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na kwamba mwaka huu 2012 uagizaji wa pulses unatarajiwa kuongezeka kwa asilimi 20 zaidi.

Chini ya  makubaliano ya kibiashara ya “Indo-Tanzania Trade Agreement” [1966 na 1975], ambapo nchi hizi mbili zimekubaliana kupanua wigo wa ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni kupitia  Joint Permanent Commission [JPC] na  Joint Trade Committee [JTC], vile vile  zimeafikiana juu ya mifumo, taratibu na itifaki mbali mbali zenye lengo la kurahisisha ushrikiano huo.

Miongoni mwa Makubaliano/Mikataba ya Kiserikali ambayo yanayotoa fursa kwa Watanzania kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi na biashara na India ni:-
(iMaboresho ya Mkataba wa kuzuia utozaji kodi mara mbili “Revised [May 2011] version of the
[1979] Double Taxation Avoidance Agreement [DTAA]”

(ii) Mpango wa Msamaha/unafuu wa Ushuru kwa baadhi ya bidhaa [Duty Free and Tariff Preference”- DFTP Scheme] uliotolewa na Serikali ya India kwa nchi zinazoendelea.
(iii) Huduma ya Mkopo na Mifuko ya Ruzuku [Line of Credit” facility “Grant Funds] inayotolewa na Serikali ya India kwa nchi zinazoendelea.
(iv) Fursa za mafunzo ya muda mfupi na mrefu zinazotolewa na Serikali ya India chini ya mipango ya “Indian Technical and Economic Cooperation [ITEC] Scholarship Programme na “the Indian Council for Cultural Relations (ICCR) Scholarship Programme”.
(v) Waziri Mkuu wa India Dr. Manmohan Singh  alipofanya ziara nchini Tanzania mnamo mwezi wa Mei, 2011, Mikataba mbali mbali ilitiwa saini. Baadhi ya makubaliano ya Mikataba hiyo ni:

 • India itatoa Ruzuku ya  US$ 100,000 Grant kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya Maabara za shule. [Money for school laboratory Equipments].
 • India itatoa Ruzuku ya US$ 10,000,000  kwa ajili ya masomo/kujenga  uwezo wa sekta za Jamii na Elimu [Capacity building on Social and Education Sectors].
 • India  imeahidi  kusaidia    kuanzisha Kituo  cha  Mafunzo  ya  Aamali  [Vocational  training  centre] Zanzibar.
 • Huduma ya Mkopo [line of Credit facility] wa US$ 180 Million kwa ajili ya Miradi ya maji ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
 • India na Tanzania zimetiliana saini Makubaliano Mpangokazi wa pamoja  [Joint Action Plan] baina ya “Small Scale Development Organisation SIDO” ya Tanzania na “National Small Industries Corporation Ltd ya India.
 • Makubaliano ya awali ya ushirikiano [Preliminary joint Venture Agreement] yametiwa saini baina ya Apollo Hospitals za India and NSSF Tanzania   kujenga Hospitali ya Apollo   mjini Dare s salaam.
 • Kuzinduliwa kwa  India-Tanzania Centre  of  Excellence in  Information and  Communication
 • Technology” mjini Dar es Salaam.
 • Vile vile kuna makubaliano ya sekta binafsi ambayo yanaweza pia kuhuwishwa na kuendelezwa ili kuimarisha ushirikiano huo. Miongoni mwao ni:
 • Makubaliano ya kuanzisha Baraza la pamoja la Biashara  “Agreement on the Establishment of Joint  Business  Council”  yaliyofikiwa  baina  ya    FICCI,  ASSOCHAM  [India]  na   Tanzania Chamber of Commerce, Industry & Agriculture –TCCIA mwaka 1997.
 • Makubaliano [MOU] ya ushirikiano baina ya “Indo-Africa Chambers of Commerce and Industry – IACCI na “Zanzibar National Chamber of Commerce Industry and Agriculture – ZNCCIA” yaliyotiwa saini mwaka 2011.
 • Hivyo, Watanzania wanaweza kufaidika zaidi na soko la India kwa kutumia fursa za makubaliano ya kibiashara zilizoainishwa hasa “Duty Free and Tariff Preference” - DFTP Scheme” ambapo
 • India inatoa fursa kwa Tanzania kuuza nchini India bidhaa zaidi ya 90, bila ushuru au kwa ushuru mdogo.

Kwa taarifa zaidi juu ya sheria na taratibu zinazolinda masuala ya biashara hapa India ikiwa ni pamoja na Sera ya uagiziaji [Import Policy], takwimu [data] za uchumi, biashara, masoko, wawekezaji, waagiziaji mikutano/makongamano na maonyesho ya biashara na uwekezaji na mengine yanayohusiana na hayo tembelea Tovuti zifuatazo:-

 1. Wizara ya Biashara na Viwanda ya India -  www.commerce.nic.in
 2. Invest Technology Division [Ministry of External Affairs] – www.mea.gov.in
 3. Directorate of General Foreign Trade – www.dgft.gov.in
 4. Indian Importers Association - www.indianimportersassociation.com
 5. Pulses Importers Association - www.pulsesindia.in
 6. India Pulses & Grains Association - www.ipga.co.in
 7. North India Importers Association - www.niia.co.in
 8. Indo-African Chamber Of Commerce & Industries - www.indoafrican.org
 9. The Federation of Indian Export Organisations - www.fieo.org
 10. Federation of International Business Association FIBA - www.intl-fiba.org
 11. The Associated Chambers of Commerce and Industry of India - www.assocham@nic.in
 12. Federation of Indian Chambers of Commerce and Industry – FICCI - www.ficci.com
 13. Confederation of Indian Industry - www.cii.in
 14. EEPCINDIA – www.eepcindia.net